Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Hali ilivyokuwa baada ya KRC Genk ya Samatta kuingia fainali (video)

on

Club ya KRC Genk ya Ubelgiji anayocheza Mtanzania Mbwana Samatta usiku wa February 6 2018 walicheza mchezo wao wa marudiano wa nusu fainali dhidi ya Kortrijk katika uwanja wao wa nyumbani Luminus Arena.

Mchezo huo KRC Genk walikuwa wanahitaji ushindi wa aina yoyote ili wafuzu kucheza hatua ya fainali ya baada ya game ya kwanza ugenini kufungwa magoli 3-2, ila usiku wa jana Mbwana Samatta akiitumikia Genk kwa dakika 90 baada ya kutoka majeruhi, imefanikiwa kufuzu yeye akiwa sehemu ya timu.

Usiku wa jana Genk wamefanikiwa kufuzu kwa ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Ibrahim Seck dakika ya 15, hivyo wanafuzu kwa ushindi wa jumla ya magoli 3-3 ila wanafuzu kwa kushinda magoli mengi ugenini, mchezo wa fainali utacheza katika jiji la Brussels.

VIDEOMagoli: Ushindi wa 4-0 wa Yanga vs Njombe Mji, Obrey Chirwa akipiga hat-trick

Soma na hizi

Tupia Comments