Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Lukaku amesainiwa na Roc Nation ya Jay Z

on

Staa wa Man United na timu ya taifa ya Ubelgiji Romelu Lakaku leo ameitangaza good news katika maisha yake ya soka, Lukaku ametangaza rasmi kusainiwa na Roc Nation Sports Agency ambayo inamilikiwa na staa wa muziki wa Marekani Jay Z.

Lukaku na mdogo wake

Baada ya kusaini mkataba huo Lukaku mbele ya mama yake mzazi sasa atakuwa akisimamiwa na Roc Nation Sports Agency katika shughuli zake zote za kisoka kama dili za matangazo ya biashara.

Lukaku akisaini mkataba mbele ya mama yake

Lukaku ambaye amesaini dili hilo akiwa New York Marekani ndio anakuwa mchezaji wa kwanza kutoka Ligi Kuu England kupata nafasi ya kuingia mkataba na Roc Nation Sports Agency inayomilikiwa na rapper Jay Z.

ALL GOALS: Simba vs Mbeya City April 12 2018, Full Time 3-1

Soma na hizi

Tupia Comments