Tangaza Hapa Ad

Mix

Nape Nnauye na RC Mongella walikua wanatazama TV, ikabidi wapige simu

on

Unamkumbuka msanii maarufu aitwae Jetman? ni msanii wa Reggae kutoka Mwanza aliyetamba na nyimbo mbalimbali lakini kwa miaka ya karibuni amekua kimya kwa zaidi ya miaka minne akiwa tu kitandani kutokana na ugonjwa wake wa kupooza mgongo.

Pamoja na hali hiyo bado hajakata tamaa na anapambana kutengeneza mziki hapohapo kitandani japo anapata maumivu makali na amekua akitafuta msaada ili akatibiwe India kwani Tanzania imeshindikana.

Leo February 14 kupitia 360 ya CloudsTV imetumia nafasi hiyo kuwaomba Watanzania kumsaidia ambapo wakati anahojiwa kwenye TV, Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na michezo Nape Nnauye alikua anatazama na akapiga simu live na kutoa ahadi ya kumsaidia.

“kwanza niwashukuru kwa kuelekeza upendo wenu na siku ya wapendanao kwa watu wenye mahitaji na kumchagua Jetman najua wapo wengi wenye mahitaji lakini walau kuonesha mfano kwa huyu mmoja na mimi kama Waziri ninayeshughulikia Sanaa nimeguswa na wito wenu”

“Nikasema niwe mtu wa mwanzo kununua biti yake na leo hii ntapita mwenyewe pale THT kwaajili ya kurecord kwahiyo nitanunua na nichukue nafasi hii kuwahamisisha Wasanii wengine tujumuike tupate zaidi ya hicho ambacho kinatakiwa ili tumsaidie mwenzetu akapate matibabu”>>> Nape Nnauye

Alipoulizwa kama hiyo beat ataitumia mwenyewe na ataimba kuhusu nini? alijibu>>>> “Nitaimba na nitawalipia wengine watano ila wawe Wasanii wadogo na sio Wasanii wakubwa lakini mimi mwenyewe nitaanza kwa kuimba kwa sababu ya siku ya leo nitaimba kuhusu upendo, unajua Dunia inakuwa sehemu nzuri yakuiishi kama watu watapendana, so ntakwenda kwenye upendo na siyo mapenzi”

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella naye aliguswa na akapiga simu Live kwenye kipindi nakuahidi Laki 5 “Nilikuwa gafla nimeingia ofisini mtu mmoja akaniambia mnazungumzia kitu kuhusu mwanza, nilipoongeza sauti nikasikia stori ya Jetman, nikampigia Ruge nikamuuliza hii kitu vipi akasema ni kweli huyu msanii yupo”

“Na mimi niseme hivi kwa sababu ni mwananchi wangu kwanza leo hii nitachukua watu wangu wanaohusika na sekta hiyo twende tukamuone lakini na mimi kwa jinsi Ruge alivyo nielewesha na mimi ntajitaidi leo hii hii tutoe Laki tano”

Ukihitaji kumchangia kwa M-PESA namba zake ni hizi hapa mtu wa nguvu 0763 48 40 06, 0757 62 62 07

VIDEO: Kijana Kinyozi aliyetobolewa macho Dar es salaam amekutana na Diamond Platnumz, tazama kwenye hii video hapa chini

Tupia Comments

Advertisement