Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Simba wamemalizana na Gendermarie nchini Djibout leo

on

Club ya wekundu wa Msimbazi Simba leo ilicheza mchezo wake wa marudiano wa Kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya wenyeji wao Gendermarie nchini Djibout, Simba ilikuwa inahitaji walau sare.

Simba katika mchezo wa kwanza uliyochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ulimalizika kwa Simba kupata ushindi wa magoli 4-0, hivyo mchezo wa leo walikuwa wanahitaji sare au kupoteza kwa chini ya magoli matatu kwa bila.

Good news ikufikie Simba licha ya kuwa katika ardhi ya ugenini wamefanikiwa kuitoa Gendermarie baada ya kuifunga goli 1-0 lililofungwa na Emmanuel Okwi dakika ya 53, ushindi huo unaifanya Simba kufuzu hatua inayofuata kwa ushindi wa jumla ya magoli 5-0.

Mastaa wa soka Bongo Niyonzima, Kaseja, Okwi, Manula na Himid wakiwa na wake zao

Soma na hizi

Tupia Comments