AyoTV

“Tulijua tutakutana na mpinzani imara tukaamua kumpa presha”-Kocha Simba SC

on

Simba SC mbele ya mashabiki wao wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 4-1, magoli ya Simba SC yakifungwa na nahodha wao John Bocco dakika ya 7, 37 kwa penati, Meddie Kagere dakika ya 84 na Chota Chama dakika ya 90, wakati Mbabanewameishia kufunga goli moja pekee kupitia Nzambe dakika ya 24, baada ya mchezo huo kocha wa Simba SC Patrick Aussems aliongea na waandishi wa habari.

“Tunajua kuwa tulikuwa tunacheza dhidi ya mpinzania mzuri hivyo tuliamua toka mwanzo kuwapa presha na tulianza vizuri uliona tulipata goli la kwanza kabla ya dakika ya nane au ya tisa, kwa bahati mbaya baada ya dakika ya 20 walipiga shuti moja lililolenga lango la kufunga goli lakini nimeridhishwa na uwezo wa wachezaji wangu baada ya kufungwa goli moja hawakukata tamaa na kuendelea kucheza”>>> Patrick Aussems 

EXCLUSIVE: Kauli ya Singida United kushindwa kulipa wachezaji, mbona wanasajili?

Soma na hizi

Tupia Comments