Michezo

Wachezaji wa Man United wameamua kumuokoa Mourinho

on

Baada ya headlines za muda mrefu kuhusiana na hatma ya kocha wa Man United Jose Mourinho kama angepoteza mchezo wa leo wa Man United dhidi ya Newcastle  katika uwanja wa Old Trafford kuwa atapoteza ajira.

Mourinho leo alikuwa na wakati mgumu zaidi toka aanze kuwa kocha wa Man United, hususani baada ya Newcastle kupata magoli mawili ndani ya dakika 10 za mwanzo, magoli yakifungwa na Kenedy dakika ya 7 na Muto dakika ya 10.

Game hadi dakika 90 zinamalizika Man United walifanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-2, magoli ya Man United yakifungwa na Juan Mata dakika ya 70, Anthony Martial dakika ya 76 na goli la ushindi lilifungwa dakika ya 90 na Alex Sanchez.

Kama Man United angepoteza mchezo huo dhidi ya Newcastle inayoshika nafasi ya pili kutoka mwisho ingekuwa fedhea kwa timu hiyo, kwani Newcastle inaonekana kuwa kibonde msimu huu na haijashinda mchezo wowote, hivyo Man United wangepata sababu ya kumuondoa Mourinho.

Matokeo ya game za EPL leo.

Msimamo wa EPL ulivyo kwa sasa.

“Simba tumewaachia, sisi hatuna presha”-Kocha wa Yanga

Soma na hizi

Tupia Comments