Michezo

Bondia Mtanzania apoteza pambano Urusi kwa kupigwa sehemu za siri

on

Bondia mtanzania Idd Mkwera amepoteza pambano lisilokuwa la Ubingwa uzito wa Kilogram 66 Welter weight nchini Urusi katika mjii wa Ekaterinburg, baada ya kupigwa round ya 3 maeneo ya sehemu za siri katika pambano la round 8 dhidi ya bondia Makhmud Agaipov kutoka Uzebekstan.

Promota wa mchezo wa ngumi Tanzania aliyekuwa ameambatana na Idd Mkwera anayejulikana kwa jina la Jay Msangi, ameeleza hujuma zilizofanyika dhidi ya bondia wake ni pamoja na kupigwa ngumi sehemu za siri lakini muamuzi hakutilia maneno, kisheria mchezo wa ngumi hauruhusu kumpiga bondia kichogoni na sehemeu za siri pia.

“Pambano hili ambalo lilikuwa la round 8 la KG 66 Welter Weight, kwa bahati mbaya naweza kusema kuwa habari sio nzuri kwamba mtanzania amepoteza round ya tatu, round ya tatu bondia Agaipov alimpiga mtanzania ngumu isiyoruhusiwa mchezoni katika sehemu za siri, baada ya kupigwa mara moja alilalamika kwa muamuzi lakini hakusikilizwa>>>Jay Msangi

Angalia Mwakinyo alivyoendeleza ubabe, kampiga Sinkala TKO round ya pili

Soma na hizi

Tupia Comments