Michezo

Utani wa Zitto Kabwe kwa Albert Msando akimuhisisha Coutinho

on

Hivi karibuni Tanzania tumekuwa tukishuhudia baadhi ya wanasiasa na wanachama wakongwe wa vyama vya kisiasa wakihama vyama vyao na kujiunga na vyama vingine huku wakitoa sababu zao mbalimbali.

Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa ACT Wazalendo Zito Kabwe amezichukua headlines kufuatia tweet yake aliyoipost twitter yake kuhusu mbrazil Philippe Coutinho anayekaribia kuihama Liverpool na kujiunga na FC Barcelona ikidaiwa kuwa anafuata makombe.

So Zitto Kabwe amehusisha tweet hiyo na utani kwa mwanasheria Albert Msando ambaye amewahi kuwa mwanasheria wao wa ACT Wazalendo lakini kwa sasa amejiunga na Chama Cha Mapinduzi CCM, Zitto Kabwe ameandika hivi katika twitter account yake

“Timu yangu ‪@LFC ‪#Liverpool imekuwa kama Chama changu ‪@ACTwazalendo. ‪@Phil_Coutinho naye kasepa kaenda zake kukutana na ‪@LuisSuarez9. Kisa? Makombe. Makombe yatakuja tu ‪@AlbertMsando

Simon Msuva amerudi Tanzania leo, alichozungumza kipo hapa

Soma na hizi

Tupia Comments