Biko Ad 2
MPTV Ad
TIC Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Zlatan amekubali yaishe, kamuandikia hivi Beckham

on

Siku moja kabla ya mchezo wa robo fainali ya World Cup 2018 staa wa soka wa zamani wa Sweden anayecheza LA Galaxy ya Marekani Zlatan Ibrahimovic kupitia ukurasa wake wa instagram alipost ujumbe wa kishabiki kati yake na Beckham.

Zlatan ni raia wa Sweden na Beckham raia wa England hivyo Zlatan alimwambia Beckham kama Sweden itashinda basi Beckham atalazimika kumnunulia chochote Zlatan kutoka katika maduka ya IKEA.

Huku Beckham yeye akimwambia Zlatan kama England itashinda basi atamchukua aende Wembley siku moja akaangalia game ya England ikicheza akiwa kavaa jezi ya England na wakati wa mapumziko watakula samaki pamoja.

Game ilimalizika kwa England kushinda magoli 2-0 dhidi ya Sweden hivyo Zlatan akaandika hivi kuashiria kuwa atatekeleza makubaliano “David Beckham nakuja na hongera” Zlatan na Beckham ni marafiki na waliwahi kucheza pamoja katika club ya PSG ya Ufaransa.

Soma na hizi

Tupia Comments