Michezo

Harry Kane kaingia kwenye vitabu vya kihistoria baada ya miaka 32

on

Moja kati ya mataifa ambayo Ligi yao inapendwa na mashabiki wengi wa soka duniani basi ni Ligi Kuu England, mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs na timu ya England Harry Kane ameingia katika vitabu vya rekodi England.

Harry Kane leo akiiongoza England katika mchezo wake wa kwanza wa Kombe la Dunia dhidi ya Tunisia, ameiwezesha timu yake kupata ushindi wa magoli 2-1, magoli ya England yote akifunga Harry Kane dakika ya 11 na 91, huku la Tunisia likifungwa na Farjan Sassi kwa penati dakika ya 35.

Baada ya kufunga magoli mawili leo, Harry Kane anaweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa England, kuwahi kufunga magoli mawili ndani ya dakika za kawaida katika fainali za Kombe la Dunia toka 1986 toka afanye hivyo Gary Lineker dhidi ya Uruguay.

Kane anafanikiwa kuifikia rekodi hiyo baada ya miaka 32 kupita, Gary Lineker pia alifunga mara mbili katika mchezo wa World Cup 1990 dhidi ya Cameroon ila ilikuwa ni katika dakika 30 za nyongeza.

Soma na hizi

Tupia Comments