Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Mahakama yamruhusu Mgombea Urais mwingine Kenya

on

Baada ya Raila Odinga kujiengua kwenye kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu wa marudio Kenya Mahakama Kuu nchini humo imeamuru mgombea urais wa chama cha Thirdway Alliance, Ekuru Aukot aliyekuwa ameshiriki uchaguzi mkuu tarehe 8 Agosti ashirikishwe kwenye uchaguzi huo ambao utafanyika Oktoba 2, 2017.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi IEBC ilikuwa imetangaza kwamba ni wagombea wawili pekee, Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee na Raila Odinga wa muungano wa National Super Alliance (Nasa) wangewania kwenye uchaguzi huo.

Dkt Aukot ameeleza kuwa amefurahia uamuzi huo na kwamba sasa watakuwa kwenye uchaguzi kwani mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alikuwa amewafungia kutoshiriki.

Ulipitwa na hii? MKEMIA MKUU: ‘Wanafunzi wanaoenda vyuoni wapimwe matumiz ya dawa za kulevya’

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement