Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Mourinho katupa dongo kwa kocha wa Chelsea

on

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho ameendeleza vita ya maneno dhidi ya kocha wa Chelsea Antonio Conte baada ya kuzungumza na waandishi wa habari baada ya game ya FA iliyomalizika kwa Man United kupata ushindi wa magoli 2-0.

Jose Mourinho baada ya game aliongea na vyombo vya habari kama ilivyokawaida lakini alitoa kauli inayosadikiwa kuwa ni kijembe kwa kocha wa sasa wa Chelsea Antoanio Conte.

Antoanio Conte.

“Simlaumu kwa kitendo chake kiukweli simlaumi kabisa nilijizungumzia mwenyewe na nina uwezo wa ku-control mapenzi yangu katika njia sahihi, kitu ambacho hakiwezi kutokea kwangu na hakitakaa kitokee kamwe ni kufungiwa kwa sababu ya kupanga matokeo kamwe hakitatokea”>>>Jose Mourinho

Kauli ya Mourinho imetafsiriwa kama ni kejeli kwa Conte ambaye amewahi kufungiwa miezi 10 kufundisha soka miaka 7 iliyopita wakati ambao alikuwa akiifundisha Siena kwani alikutwa na tuhuma za upangaji wa matokeo.

George Weah amemtumia mualiko kocha Arsene Wenger

Soma na hizi

Tupia Comments