Tangaza Hapa Ad

AyoTV

‘Tulishafunga mjadala kuongelea maswala ya Lord Eyes’ – Joh Makini

on

Inawezekana wewe ni miongoni mwa mashabiki waliotamani kufahamu WEUSI watasema nini kuhusu rapper Lord Eyes ambaye kwa karibuni ameonekana akitumbuiza mwenyewe kwenye majukwaa ya FIESTA 2016 bila kuambatana na WEUSI kama ilivyokua kipindi cha nyuma.

Kwenye Interview na millardayo.com Joh Makini amesema kwa sasa wamefunga mjadala wa kumuongelea Lord Eyez >>>Tulishafunga mjadala kuongelea kuhusu maswala ya Lord Eyes lakini tutakapokua na ishu yoyote kutoka kwa Lord Eyes tutawaambia’

Kuhusu WEUSI kusainisha Wasanii chini ya lebo Joh amesema ‘ni mapema kusema tuna mpango wa kusainisha lakini tuna Wasanii wachanga tuko nao tunawa-support na kuwashauri na tunapiga nao kazi katika staili ambayo kama tungekua na sisi tunataka hizo kiki za kusema tumeanza kusaini watu tungefanya hivyo, hata hivyo ni mapema kusema kuhusu kusaini Wasanii kwa sasa

VIDEO: Tazama Nikki wa II alivyotangaza Lord Eyez kusimamishwa WEUSI miaka miwili iliyopita

VIDEO: Ulimis kuona alichofanya Lord Eyes kwenye FIESTA 2016 Dar es salaam? tazama hii video hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement