Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Rais Magufuli aagiza Kaya 1900 waliovamia Uwanja wa Ndege kutoondolewa

on

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amerejea nchini leo February 24, 2018 akitokea nchini Uganda ambako amehudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliomalizika jana Mjini Kampala.

Katika uwanja wa ndege wa Mwanza Rais Magufuli amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella aliyeongozana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Antony Dialo.

Rais Magufuli amezungumza na wafanyakazi wa uwanja wa ndege ambapo ameahidi kuwa Serikali itafanyia kazi mahitaji ya kujengwa kwa jengo la abiria pamoja na ujenzi wa uzio ili uwanja wa Mwanza uwe na hadhi ya kimataifa na hivyo kuiwezesha nchi kupata mapato zaidi.

President Magufuli amezungumzia changamoto ya ndege za kubeba minofu ya samaki kutotumia uwanja wa Mwanza ambapo amesema Serikali itafanyia kazi jambo hilo na kulitafutia ufumbuzi haraka ili ndege hizo zitumie uwanja huo na kuiingizia nchi mapato.

Aidha, Rais Magufuli amesema anasubiri ripoti ya Wizara ya Ardhi kuhusu wananchi waliovamia uwanja wa ndege wa Mwanza lakini amebainisha kuwa Serikali haiwezi kukimbilia kuondoa kaya zaidi ya 1,900 zinazodaiwa kuvamia eneo hilo na badala yake itaangalia njia bora ya kufanya.

Hata hivyo ametaka wananchi waliopo katika eneo hilo wasiendeleze makazi yao wakati uamuzi wa Serikali unasubiriwa.

“Bahati nzuri Naibu Waziri wa Ardhi upo hapa, kafanyieni kazi changamoto hii na mnipe ripoti” -Rais Magufuli.

Baada ya kutoka uwanja wa ndege wa Mwanza Rais Magufuli ameelekea nyumbani kwake Chato Mkoani Geita kwa mapumziko.

RPC KINONDONI AMEZUNGUMZA KUHUSU MAJERUHI WA RISASI WALIOPO OYSTERBAY Polisi
Soma na hizi

Tupia Comments