Tangaza Hapa Ad

AyoTV

AUDIO: KRC Genk imeomba TFF ifanye hivi kabla ya kumtumia Samatta Jumamosi

on

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Jumamosi ya September 3 2016 itacheza mchezo wa kukamilisha ratiba ya michuano ya kuwania kufuzu kucheza AFCON 2017 dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria, Samatta ambaye ataungana na timu Lagos akitokea Ubelgiji limetoka angalizo kutoka katika klabu yake ya KRC Genk.

Afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania TFF Alfred Lucas amethibitisha kutumwa kwa taarifa kutoka KRC Genk Ublegiji taarifa ambayo imeelekezwa kwa daktari wa Taifa Stars, Richard Yomba kuhusiana kumpima Mbwana Samatta kabla ya kucheza mchezo wa Jumamosi dhidi ya Nigeria kwani ametumika bila kupumzika.

“Kauli hii imetokana na hali ya mchezaji mwenyewe kwani Genk walijua Samatta atapumzika ila kaitwa timu ya taifa na katika wiki ya FIFA imebidi wamuachie aje, lakini wameomba apimwe kabla ya kutumika au kufanya mazoezi kwani wao vipimo vyao vinaonesha kachoka”

GOAL AND HIGHLIGHTS: YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement