Tangaza Hapa Ad

Mix

VIDEO: Mkurugenzi CUF aliyedaiwa kutaka kutekwa asimulia tukio lilivyokuwa, Prof. Lipumba atajwa

on

Baaada ya kuwepo kwa taarifa za wanachama watatu wa chama cha wananchi CUF kuhojiwa na jeshi la polisi Dar es salaam kwa tuhuma za kumteka mkurugenzi wa uchumi na fedha wa chama hicho, Jorah Bashange.

Leo September 17 2016, baadhi ya viongozi wa chama hicho akiwemo mkurugenzi wa uchumi na fedha anayedaiwa kutekwa, Jorah Bashange amekutana na waandishi wa habari na kusimulia tukio lilivyokuwa…..

>>>’Asubuhi nilitoka nyumbani kwangu nilipotoka nje kama hatua 20 kulikuwa na gari moja ya Tinted Noah,  nilipotoka kuipita kidogo mtu aliyekuwa ndani akashuka na akatoa kitambulisho akakionyesha na kukirudisha palepale kuwa ni askari polisi wa buguruni nahitajika kituoni’;-Jorah Bashange.

>>> ‘Nilipomcheki nilimtambua kuwa ni miongoni mwa mabaunsa anaowatumia Prof. Lipumba, nilifanya kwenda mbele kidogo ili asiniingize kwenye gari na sikujua kama ndani ya gari kuna watu wengine, tukaangaishana naye kwa kama dakika 10 baadae akawaita wenzake’:-Jorah Bashange.

JE CUF WATAKA A MEZA MOJA NA PROF. LIPUMBA? MAJIBU YAMETOLEWA HAPA KWENYE HII VIDEO

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement