Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Idadi ya viajana wenye miaka 24 hadi 36 wanaoishi kwa mama zao imeongezeka

on

Leo May 13, 2018 nakusogezea ripoti iliyotolewa na Zillow ambao unasema Idadi ya vijana wenye umri kati ya miaka 24 hadi 36 ambao wanaendelea kuishi nyumbani kwao na mama zao imeongezeka zaidi katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Ripoti ya Zillow imesema Mji wa New York, nchini Marekani ni miongoni mwa miji 5 yenye idadi kubwa zaidi ya vijana kati ya miaka 24 hadi 36 wanaoendelea kuishi nyumbani na mama zao.

Ripoti hiyo imesema kwamba asilimia 22.5 au vijana wapatao milioni 12 bado wanaishi na mama zao kote nchini Marekani. Katika miji ya New York, Los Angeles, Riverside na Jimbo la California zaidi ya asilimia 30 ya vijana wenye umri kati ya 24 hadi 36 bado wanaishi na mama zao.

LIVE MAGAZETI: Msako mkali waja, Biashara ya Viroba yashamiri upya

Soma na hizi

Tupia Comments