Tangaza Hapa Ad

Top Stories

EXCLUSIVE: “Nimefikiria hii gari isiwe ya Luxury nataka niifanyie biashara ya Uber”

on

Moja ya stori ambayo ilikuwa gumzo kutoka Kanda ya Ziwa hasa katika Mkoa wa Geita ilikuwa ni kuhusu Mkurugenzi wa Shule za Sekondari za Waja Mkoa wa Geita, Eng. Chacha Wambura kutoa zawadi ya magari kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao hasa masomo ya Sayansi na kutajwa kwenye TOP TEN Kitaifa.

Edina Meala ni mmoja wa wanafunzi hao ambaye ameshika nafasi ya Tisa Kitaifa katika matokeo ya mtihani wa Kidato cha Sita 2017, Ayo TV na millardayo.com zimempata kwenye EXCLUSIVE interview ambapo ameeleza atalitumia vipi gari lake hilo jipya.

Edina ameeleza kuwa gari hiyo aliyoipata anataka aitumie kufanya biashara ya Uber ili imsaidie gharama mbalimbali zitakazomkabili pindi atakapoanza masomo yake ya chuo kikuu.

Ulipitwa na hii? CRDB Oysterbay Branch yasherehekea wiki ya huduma kwa wateja

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement