Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: Sababu za Waziri Nape kuvifungia vituo vya Radio 5 na Magic Fm

on

August 29 2016 Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye ametangaza kuvifungia vituo viwili vya radio kwa muda usiojulikana ambavyo ni Magic Fm ya Dar es salaam na Radio 5 ya Arusha kwa makosa ya kutangaza na kutoa habari za kichochezi.

Waziri Nape amesema…>>>’Nimevifungia vituo viwili vya radio ambavyo ni Radio 5 Arusha na Magic Fm Dar kwa muda usiojulikana kwa kosa la uchochezi, hadi sasa nimeelekeza kamati ya maudhui kuviita vyombo hivyo na kuwasikiliza kwa kina kisha kunishauri hatua zaidi ya kuchukua

Adhabu hii ya kuvifungia kwa muda vituo hivyo viwili inaanza leo August 29 2016 hadi pale kamati itakapomaliza kazi yake, kimsingi radio zote mbili kwa pamoja wametangaza na kutoa habari ambazo zina uchochezi ndani yake‘ –Waziri Nape Nnauye

Unaweza kuendelea kumsikiliza kwenye hii video hapa chini…

KILICHOJIFICHA MAGUFULI NA LOWASSA WALIPOKUTANA, MVUA YA RISASI ZAIDI YA 50 ILIVYOCHAKAZA NYUMBA DAR

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement