Top Stories

Alichotabiri Nguruwe kuhusu Nigeria Kombe la Dunia

on

Leo June 14, 2018 Nguruwe anayejulikana kama Mystic Marcus kutoka nchini Uingereza ametabiri kuwa timu ya taifa ya Nigeria itafika nusu fainali ya mashindano ya Kombe la Dunia nchini Urusi.

Nguruwe huyo mwenye miaka 8 amewahi kutabiri mshindi wa Kombe la Dunia mwaka 2014 na mshindi wa Wimbledon katika mchezo wa Tenisi.

Tofauti na utabiri huo Nguruwe huyo aliwahi pia kutabiri ushindi wa Urais wa Donald Trump pamoja na kujitenga kwa nchi ya Uingereza katika Umoja wa Ulaya.

Kwa upande mwingine Marcus ametabiri kuwa timu ya taifa ya Uingereza itafanya vibaya katika michuano hiyo huku akitabiri timu za taifa ya Ubelgiji na Uruguay kuvuka hatua ya makundi.

BAJETI KUU YA SERIKALI: Wananchi wafunguka wanachohitaji kiwepo

Soma na hizi

Tupia Comments