Top Stories

Kusaga kafunguka “namiliki Redio zote za Vijana, hakuna Staa bila Clouds”

on

Leo December 4, 2018 Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga amefunguka juu ya ishu ya umiliki wa Vituo mbalimbali vya Redio na TV nchini nakusema anamiliki redio zote zinazomilikiwa na vijana nchini.

Akizungumza katika Kipindi cha Clouds 360 Kusaga “Namiliki Redio zote za vijana kwa namna moja au nyingine. Naamini kwenye ushirika na hivyo kuna biashara nyingi pamoja na Redio nitaendelea kuzianzisha kwa kushirikiana na vijana kwa sababu hilo lilikuwa lengo la Clouds tangu zamani”

Kusaga amesema kuwa anashirikiana na radio nyingine za mikoani kama Safari FM ya Mtwara na Jembe FM ya Mwanza

Pia Kusaga amesema  “Utake usitake bila Clouds hakuna Staa yeyote angetokea, hata watukane waseme nini ila bila Clouds wasingekuwa walipokuwa”

Kabla ya kutoa tamko hilo, kulikuwa na maneno kuwa Kusaga ndiye mmiliki wa vituo vya Wasafi TV na Wasafi FM.

MSIMAMO WA CCM JUU YA ISHU YA MEMBE NA DK. BASHIRU “CHUKI, UHASAMA” VYATAJWA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA 

 

Soma na hizi

Tupia Comments