Top Stories

Rais wa TLS ataja vitu vinavyomharibu Mwanaume, amuweka wazi Mwanamke hatari

on

Rais wa Chama cha Mawakili nchini (TLS), Fatma Karume ametoa maoni yake juu ya kitu kinachowaharibu wanaume huwa ni pesa na madaraka na si kingine, wengi wao hugeuka na kuanza kufanya vitendo vya kikatili.

Ameandika hivi katika Twitter yake “Vitu viwili vinamharibu mwanaume dhaifu, pesa na madaraka. Akishayapata hayo mawili anapofuka macho na anakua kiziwi ispokua pale anaposifiwa tu”.

Pia akaandika tena “Mwanamke dhaifu anakua hatari pale anapokua anauchu wa pesa au madaraka. Anaweza kufanya chochote ili apate haya. See Gender Neutral”

Fatma anaandika haya wakati jamii ikiwa katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na Utafiti wa Shirika la Afya Duniani (WHO) umesema mwanamke mmoja katika kila wanawake watatu  amewahi kufanyiwa ukatili wa kijinsia, kimwili, kingono au kisaikolojia.

KESI YA AKWILINA: Mbowe, Matiko Gerezani, Heche, Mdee waeleweka Mahakamani

Soma na hizi

Tupia Comments