Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Aliyemuua ndugu yake Rihanna afikishwa Mahakamani

on

Leo January 5, 2918 Mwanaume mmoja amekamatwa na kufunguliwa mashtaka ya mauaji ya Tavon Kaiseen Alleyne, 21 ambaye ni ndugu wa mwanamuziki wa kimataifa Rihanna.

Taarifa zilizotolewa na Nation News zimesema, “kijana huyo anafahamika kama Shawayne Dashawn Williams ana umri wa miaka 23, amefunguliwa mashtaka ya mauaji hayo ya Alleyne ambayo yametokea wiki iliyopita katika sikukuu ya Christmas.”

Shawayne amefikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza na kesi hiyo imeahirishwa na mtuhumiwa amerudishwa gerezani huku hukumu ya kesi hiyo ikipangwa kutolewa January 31, 2018.

Kabla ya tukio marehemu Alleyne alikuwa akitembea karibu na nyumba yake majira ya saa 1 usiku kabla ya kufatwa na mtu asiyefahamika na kisha kupigwa risasi. Hata hivyo Alleyne alikimbizwa hospitali ya Queen Elizabeth iliyopo Bridgetown lakini alifariki dunia.

Wakati huo huo marehemu Tavon Alleyne alikuwa na Rihanna saa moja kabla ya kufariki dunia wakisherehekea pamoja sikukuu ya Christmas.

MSIBA: MWANAMUZIKI MKONGWE WA DANSI AFARIKI DUNIA

FULLVIDEO: BABU SEYA NA PAPII KOCHA RASMI WAINGIA STUDIO, WAZUNGUMZA HAYA

Soma na hizi

Tupia Comments