AyoTV

Abdi Kassim bado anakipiga, asema Canavaro kashawishiwa kustaafu

on

Kiungo Abdi Kassim Babi ambao wengi wamemzoea kwa jina la Ballack wa Unguja bado anaendelea kukipiga katika Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019 mzunguuko wa pili tutamuona katika club ya African Lyon akitokea Mawenzi FC ya daraja la kwanza kwa mkataba wa miezi sita.

Abdi Kassim ni moja kati ya wachezaji ambao wamewahi kucheza soka la kulipwa katika nchi za Malaysia lakini nyumbani Tanzania pia amewahi kucheza Mtibwa Sugar, Yanga SC na Azam FC pia timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars na timu ya taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’

Babi amewahi kucheza na nahodha wa Yanga wa zamani ambaye kwa sasa ni meneja wa Yanga Nadir Haroub Canavaro ambaye mwenzake amestaafu ila yeye bado anakipiga na anasema anaweza kucheza soka hata miaka mitano hadi sita tulipomuuliza kuhusu Canavaro akasema mwenzake alishawishiwa kustaafu.

“Cha msingi mimi mwili wangu ndio naufuata sio akili, mwili unataka na akili haina shida basi nacheza tu kwa sababu watu wengi wanashangaa kwa nini Babi unasikiliza maneno ya watu, kwa hiyo bado nina muda wa kuendelea kucheza soka”>>> Abdi Kassim Babi

“Kabla ya maamuzi hayo ya kustaafu mimi alinipigia simu kwa jinsi alivyokuwa ananielezea kuwa anataka kustaafu soka nikagundua kuwa mzunguuko wa watu unaomzunguuka ulikuwa ni mkubwa na wote unamshauri kuwa acha mpira, kwa hiyo ile ikawa imeenea Tanzania nzima akawa yeye mwenyewe hana nguvu lakini kwa jinsi tulivyokuwa tunazungumza maamuzi yake yalikuwa 50/50”>>>Abdi Kassim Babi

Mpenja katangaza goli kabla ya kona kupigwa, ataomba kutotangaza game za timu yake

Soma na hizi

Tupia Comments