Michezo

Giroud ameamua kuizungumzia ishu ya Arsenal kumuacha Jack Wilshere

on

Mshambuliaji wa zamani wa Club ya Arsenal anayeichezea club ya Chelsea kwa sasa Oliver Giroud ameamua kufunguka na kueleza ukweli wa anachokiamaini kuhusiana na staa wa Arsenal Jack Wilshere ambaye imethibitishwa kuwa anaondoka timu hiyo.

Giroud ameamua kufunguka na kueleza kuwa Arsenal imefanya makosa sana kutangaza kuachana na Jack Wilshere ambaye amedumu katika club ya Arsenal kwa miaka takribani 17, Wilshere mwenye umri wa miaka 26 alishindwa kufikia makubaliano na Arsenal baada ya kuja kwa kocha mpya Unai Emery.

“Kwangu ilikuwa ni habari kubwa na habari ya uzuni kusikia Jack Wilshere anaondoka Arsenal, kwa sababu ni rafiki, Jack ni mchezaji mzuri na anakipaji kwa bahati mbaya alikuwa na majeruhi sana lakini msimu uliopita alirudi vizuri na kucheza vizuri, Arsenal wamepoteza mchezaji mzuri na naimani Jack atarudi akiwa na club nzuri tu”>>>Giroud

Kama utakuwa unakumbuka Oliver Giroud ambaye kwa sasa anaitumikia timu yake ya taifa ya Ufaransa katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Urusi, aliondoka Arsenal mwezi January baada ya kuitumikia kwa miaka sita na kujiunga na Chelsea ambayo anaitumikia hadi sasa.

Haji Manara kapenda usiku wa VPL ila kafunguka wasiwasi wake

Soma na hizi

Tupia Comments