Michezo

Juventus wametuma ofa hii kwa Liverpool ili wamnase MO Salah

on

Baada ya club ya Juventus ya Italia kukamilisha usajili wa kihistoria kwa kufanikisha zoezi la kumleta Cristiano Ronaldo kutokea Real Madrid ya Hispania na kujiunga na Juventus kwa dau la pound milioni 100, club ya Juventus imepanga kuingia tena kwenye rekodi za usajili mwisho wa msimu.

MO Salah

Juventus sasa wanadaiwa kuwa wapo katika mchakato wa kutuma ofa nono kwa staa wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri Mohamed Salah ili ajiunge nao mwisho wa msimu, Juventus tayari wameripotiwa kutuma ofa ya pound milioni 44 kwa Liverpool na kuwapa Paulo Dybala ili wapewe Mohamed Salah.

Paulo Dybala

Ofa hiyo ya Juventus inatajwa kuwa kubwa kiasi cha kudaiwa kuwa Liverpool hawawezi kuikataa, kwani kiasi hicho cha pesa na thamani ya Paulo Dybala ni sawa au zaidi ya pound milioni 100, hivyo inatajwa kuwa sio rahisi kwa Liverpool kuikataa ofa hiyo ukizingatia uwezo wa muargentina Pauolo Dybala.

Imeshinda Simba SC tabu kaipata JB wakati wa kutoka

Soma na hizi

Tupia Comments