Biko Ad 2
MPTV Ad
TIC Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Juan Cuadrado baada ya kukubali kumpa jezi namba 7 Ronaldo

on

Moja kati ya uhamisho uliokuwa unasubiriwa kwa hamu ni uhamisho wa staa wa soka wa kimataifa wa Ureno Cristiano Ronaldo kutoka Real Madrid na kujiunga na club ya Juventus ya Italia, hiyo ni baada ya kudumu na Real Madrid kwa miaka tisa.

Ronaldo amejiunga na Juventus akitokea Real Madrid kwa mkataba wa miaka minne kwa dau euro milioni 100 ambapo zitaongezeka euro milioni 12 katika kipindi cha miaka miwili baadae, hivyo baada ya kusaini ni wazi Ronaldo atatumia jezi yake namba saba ambayo amekuwa akiitumia miaka mingi.

Jezi namba saba kwa Juventus ilikuwa inavaliwa na Juan Cuadrado na baada ya Ronaldo kutangazwa rasmi kujiunga na Juventus, Cuadrado amekubali kubadili namba ya jezi na kumpa namba 7 Ronaldo “Ni baraka sana kutoa kuliko kupokea”

Haji Manara kaeleza sababu za kuwasajili Wawa, Dida na Kagere

Soma na hizi

Tupia Comments