Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Dili jipya la staa wa zamani wa Liverpool Steven Gerrard

on

Usiku wa May 3 2018 ziliripotiwa taarifa zisizo rasmi kuwa kiungo wa zamani wa Liverpool ambaye kwa sasa ni kocha wa mpira wa miguu Steven Gerrard kuwa yupo katika mazungumzo na viongozi wa club ya Rangers FC ili kumrithi Graeme Murty.

Leo zimetoka taarifa rasmi kuwa Steven Gerrard amekubali kusaini mkataba wa miaka minne wa kuifundisha Rangers FC na Gary McAllister ndio atakuwa msaidizi wake na Tom Culshaw na kocha wa viuongo Jordan Milsom ndio watakuwa sehemu ya benchi lake la ufundi.

Kama utakumbuka vizuri Steven Gerrard aliwahi kuichezea Liverpool kuanzia academy mwaka 1989 na mwaka 1998 alianza kucheza timu ya wakubwa ya Liverpool hadi mwaka 2015 na baadae kujiunga na club ya LA Galaxy ya Marekani na kucheza kwa msimu mmoja pekee wa 2015/2016 ila amecheza England timu ya taifa kuanzia timu za vijana 1999-2000 na wakubwa hadi 2014.

VIDEO: Mbwembwe za Haji Manara uwanjani baada ya ushindi wa Simba vs Yanga

Soma na hizi

Tupia Comments