Tangaza Hapa Ad

Michezo

PICHA: Baada ya Pogba kutengenezewa viatu kwa ajili ya Man City, Nike wamemtengenezea Rooney

on

Ni siku moja imepita toka kampuni ya vifaa vya michezo ya kijerumani Adidas kutoa kiatu maalum atakachovaa mchezaji ghali zaidi duniani Paul Pogba katika mechi dhidi ya Man City September 10 katika dimba la Old Trafford.

September 6 2016 kampuni ya vifaa vya michezo ya kimarekani ambayo ina mkataba wa kibiashara na nahodha wa Man United Wayne Rooney wamemtengenezea kiatu nahodha huyo kwa ajili ya mchezo wa derby dhidi ya wapinzani wao wa mji mmoja Man City.

Hata hivyo mchezo wa Man United dhidi ya Man City utakaochezwa katika uwanja wa Old Trafford, unatajwa kuwa na mvuto kutokana na kocha wa Man United Jose Mourinho na kocha wa Man City Pep Guardiola kuwa na uadui mkubwa na ndani ya uwanja toka wakiwa Hispania, hivyo watakuwa wanakutana  tena kwa mara ya kwanza katika ardhi ya England.

37F32FBE00000578-3774990-image-a-49_1473115817460

GOAL AND HIGHLIGHTS: YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement