Tangaza Hapa Ad

Mix

Walichoandika Watu maarufu Tanzania baada ya Makonda kutoa orodha

on

February 2 2017 mkuu wa mkoa Dar es salaam alitangaza orodha ya wanaotuhumiwa kuuza dawa za kulevya kwenye jiji la Dar pamoja na watu maarufu wanaotuhumiwa kutumia dawa za kulevya ambapo wakati hilo likiendelea mastaa mbalimbali wa Tanzania waliliendeleza gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

  1. Ommy Dimpoz alipost picha ya Harmorapa na kuandika “PALE UNAPOSUBIRIA JINA LAKO LITAJWE NA MAKONDA LIkE…..”

2 Mtangazaji wa CloudsFM Soudy Brown alitweet “NIPO KWENYE MAOMBI MAZITO, ILI CKU MAKONDA AKIJAKUTAJA LIST YA WAMBEA BASI JINA LISAHAULIKE, SHILAWADU MNISAIDIE”

3 Msanii wa bongofleva Madee alitweet “MLIOTAJWA  NA RC MFIKE MAPEMA PALE POST STESHENI BILA KUKOSA HUWEZI JUA LABDA KUNA SHOW MNAPEWA MSIWE WAOGA!!!!”

4 Mchekeshaji Joti aliweka kipande cha Video kikimuonyesha Jamaa aliyechoka akitoka jasho Huku anajipepea na kuandika “UNAPOSIKIA LIST IMETOKA NA HAUPO”

5 Comedian Indris Sultan kapost picha iliyo editiwa akiwa na Beyonce “BORA NITAFUTWE NA JAYZ LAKINI SIO PAUL MAKONDA”

6 Dj choka naye aka Tweet hii “BADO NAWAZA MAKONDA ANGETAJA WAVUTA BANGI MUDA HUU CENTRAL POLICE INGEKUWAJE”

FULL VIDEO: Tazama hapa chini Paul Makonda akiwataja wanaotuhumiwa kwa dawa za kulevya

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement