Tangaza Hapa Ad

Michezo

Majibu ya wakala wa Toure kuhusu sharti la Pep Guardiola

on

Septemba 20 2016 jina la kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast anayeichezea Man City Yaya Toure amerudi kwenye headlines baada ya kutangaza kustaafu timu ya taifa, lakini kubwa linalofanya jina lake liandikwe sana leo ni pamoja na mabishano ya wakala wake Dimitri Seluk na kocha Pep Guardiola.

Guardiola alianza kuongea leo kwenye vyombo vya habari kuwa wakala wa Yaya Toure aombe radhi kutokana na kauli alizozitoa kuhusu Man City hususani yeye ili mteja wake Yaya Toure aweze kucheza, baada ya wakala wa Toure Dimitri Seluk kufikiwa na taarifa hizo amemjibu Guardiola.

Mtu wangu wa nguvu naomba nikusogezee kauli za Pep Guardiola na Dimitri Seluk zinazotafsiriwa kama ni mabishano ya wawili hao.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Yaya Toure ambaye alijiunga na Man City mwaka 2010 akitokea FC Barcelona alipokuwa akikosa nafasi chini ya utawala wa Guardiola, amecheza mechi moja pekee dhidi ya Steau Bucharest toka kuanza kwa msimu katika mechi zaidi ya nne walizocheza Man City msimu huu.

ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement