Tangaza Hapa Ad

Michezo

PICHA: Simba yaiadhibu Polisi Dodoma mbele ya waziri Nape na naibu Spika Tulia

on

Ligi Kuu soka Tanzania bara imesimama kwa baadhi ya michezo kuahirishwa kutokana na timu husika kutoa wachezaji wengi katika kikosi cha Taifa Stars kilichopo Nigeria kupambana na wenyeji wao katika mchezo wa kukamilisha ratiba ya michuano ya kuwania kufuzu AFCON 2017.

IMG_0082

Wakati baadhi ya michezo ya Ligi Kuu ikiendelea Simba ambao ni moja kati ya vilabu vilivyoahairishiwa michezo kutokana na kutoa wachezaji wake katika timu za taifa, imecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Polisi Dodoma katika uwanja wa Jamhuri Dodoma, mchezo ambao ulihudhuriwa na wa naibu spika wa bunge DK Tulia Ackson na waziri wa mwenye dhamana ya michezo Nape Nnauye.

IMG_0101

Katika mchezo huo ambao ulihudhuriwa na mashabiki wengi wa Dodoma kutokana na kuwa na kiu ya kuzikosa Simba na Yanga zikija katika uwanja wao wa Jamhuri, mchezo ulimalizika kwa Simba kuwaadhibu Polisi Dodoma wanaoshiriki Ligi daraja la kwanza kwa goli 2-0, magoli ya Simba yalifungwa na Abdi Banda dakika za nyongeza kabla ya kwenda mapumziko na Saidi Ndemla dakika ya 60.

IMG_0054

Waziri Nape akiongea na afisa habari wa Simba Haji Manara

IMG_0049

Naibu Spika DK Tulia alipokuwa anawasili uwanjani

ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement