DSTV


Tangaza Hapa Ad

Michezo

Azam FC imelazimishwa sare na vibonde wa Yanga Mapinduzi Cup 2017

on

Azam FC leo January 4 2017 iliingia katika uwanja wa Amaan Zanzibar kucheza mchezo wao wa pili wa Kombe la Mapinduzi 2017 dhidi ya Jamhuri ya Pemba, Azam FC ambao ni Mabingwa mara mbili wa michuano hiyo wameshindwa kupata matokeo dhidi Jamhuri.

Azam FC leo wamelazimishwa suluhu na Jamhuri ambao walifungwa 6-0 katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Yanga, kitu ambacho kilifanya waanze kuonekana kama vibonde katika michuano hiyo, wengi hawakutegemea kuona Azam FC wakipata ushindani mkali kutoka kwa Jamhuri.

screen-shot-2017-01-04-at-11-32-40-pm

Kwa sasa Azam FC ambao wapo Kundi B lenye timu za Yanga, Zimamoto na Jamhuri, wapo nafasi ya pili wakiwa na point 3 huku Yanga wakiongoza kwa point sita, Azam FC sasa watakuwa na kazi ya kuwania point tatu January 7 dhidi ya Yanga katika uwanja wa Amaan saa 20:15.

ALL GOALS: JKT Ruvu vs Yanga December 17 2016, Full Time 0-3

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement