Tangaza Hapa Ad

Michezo

Ushindi dhidi ya Yanga ulioifanya Stand United kuendelea na rekodi hii

on

Ligi Kuu soka Tanzania bara iliendelea leo Septemba 25 2016 kwa Mabingwa watetezi wa Ligi hiyo klabu ya  Dar es Salaam Young Africans kushuka katika uwanja wa CCM Kambarage kucheza na wenyeji wao Stand United katika mchezo wao wa 5 wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2015/2016.

img_3921

Kwa upande wa Stand United waliingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kutoruhusu kufungwa katika michezo yao mitano kabla ya kucheza mchezo wao wa 6 dhidi ya Yanga , wakati Yanga waliingia katika uwanja huo wakiwa na rekodiya kutofungwa mchezo hata mmoja, huku wakiwa wameruhusu sare 1 dhidi ya Ndanda FC pekee katika michezo yao mitano.

img_3901

Katika mchezo huo ambao Stand United walikuwa wanadhaniwa kama dhaifu dhidi ya bingwa mtetezi Yanga, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Pastory Athanas dakika  ya 62 na kuifanya ikae nafasi ya pili katika msimamo wa VPL kwa kufikisha point 12 na Yanga kuwa nafasi ya 3 wakiwa na point 10.

img_3960

GOALS: TP Mazembe vs Yanga August 23 2016, Full Time 3-1 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement