Tangaza Hapa Ad

Michezo

Refa wa kike Hispania kasimamisha mechi na kuamuru shabiki atoke uwanjani, kisa?

on

Moja kati ya stori zinazogonga vichwa vya habari vya michezo ni pamoja na hii ya refa wa kike kutokea Ligi daraja la pili  ya Catalan Marta Galego kuamua kumtoa shabiki uwanjani kutokana na kutoa lugha ya ubaguzi wa kijinsia dhidi ya yake.

Marta Galego alisimamisha mchezo kwa dakika 3 kabla ya kuanza tena kutokana na shabiki kumwambia aende akaoshe vyombo hiyo ni kauli ambayo ilitolewa na shabiki kutokana na kutofurahishwa na maamuzi ya refa huyo, hapo ndio alipoamua kusimamisha mechi na kuamuru shabiki huyo atolewe nje.

Kitendo cha refa huyo aliyekuwa anachezesha mchezo kati ya UE Valls dhidi ya Cambrils Unió kuamuru shabiki huyo UE Valls atolewe kiliwashangaza wengi na kumpongeza, kwani mara nyingi refa huwa anawaadhibu wachezaji na watu wa benchi la ufundi la timu fulani kwa kutoa kadi na si shabiki kama alivyofanya Marta Galego.

GOAL AND HIGHLIGHTS: YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement