Tangaza Hapa Ad

Michezo

VIDEO: Ushindi wa 3-1 wa Morocco dhidi ya Togo AFCON 2017

on

Baada ya michezo miwili ya Kundi C kuchezwa leo Janury 20 2017 Oyem Gabon, msimamo wa kundi hilo bado unaendelea kuwa wazi kwa timu zote nne kuwa na nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali, Kundi C lina timu za DR Congo, Morocco, Ivory Coast na Togo.

Lakini matokeo ya mchezo wa pili wa Kundi hilo uliyomalizika kwa Morocco kupata ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Togo, umezidi kuliweka wazi Kundi hilo na licha ya DR Congo kuongoza kwa point nne akifuatiwa na Morocco mwenye point 3, Ivory Coast point 2 na Togo point moja, timu zote hizo zinaweza kufuzu na michezo yao ya mwisho ndio itaamua.

Togo inayoshika mkia mchezo wao mwisho itacheza dhidi ya DR Congo mwenye point nne na ikimfunga atakuwa kamfikia wakati, Ivory Coast na Morocco timu itakayopata ushindi itakuwa imefuzu hatua ya robo fainali moja kwa moja pasipo kutegemea matokeo ya mchezo wa DR Congo na Morocco.

Mchezo wa Togo uliyomalizika kwa Morocco kupata ushindi wa magoli 3-1, magoli yao yalifungwa na Aziz Bouhaddouz dakika ya 15, Romain Saiss dakika ya 21, Youssef En Nesyri dakika ya 72, wakati goli pekee la Togo lilifungwa na Mathew Dossevi dakika ya 5 ya mchezo.

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement