Michezo

Samatta ameifungia magoli mawili KRC Genk dhidi ya Waasland-Beveren

on

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayeichezea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta usiku wa November 30 2016 ameingia kwenye headlines baada ya kufanikiwa kuiongoza timu yake ya Genk kupata ushindi dhidi ya Waasland-Beveren.

Samatta akiwa na KRC Genk katika uwanja wa ugenini amefanikiwa kufunga magoli mawili katika ushindi wa goli 3-1, Samatta alifunga goli la kwanza dakika ya 15 goli la pili dakika ya 42 kabla ya mnigeria Wilfred Ndindi kufunga goli la tatu dakika ya 80.

Wenyeji wa mchezo huo Waasland-Beveren walifanikiwa kupata goli la kufutia machozi dakika ya 89, kupitia kwa mchezaji wao Zinho Gano, huo ulikuwa ni mchezo wa Kombe la Croky.

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments