Tangaza Hapa Ad

AyoTV

Hans alimfata Refa kuuliza kwanini alimpa red card lakini akakataa kuongea nae

on

Kwenye mechi ya Yanga vs Ruvu Shooting ulimalizika kwa Yanga kuchukua ushindi wa goli 2-1 ambapo hata hivyo kocha muholanzi wa Yanga Hans van Pluijm aliopewa kadi nyekundu na kwenda kukaa jukwaani na baadae hakutaka kuongelea kuhusu kadi hiyo.

Leo AyoTV imempata na akakubali kusema yafuatayo >>> “Ni kweli jana nilipewa kadi nyekundu na kwa bahati mbaya katika maisha yangu ya soka toka nacheza hadi ukocha sikuwahi kuonyeshwa kadi ya njano au nyekundu na nimeshangazwa sana, nilipomuuliza refa ni kosa gani limefanya nitolewe katika benchi hakutaka kuongea na mimi”

“Lakini baada ya mechi timu meneja wangu alikuja kwangu na kuniambia nimepewa kadi kwa sababu nilimsukuma refa kitu ambacho sio kweli, lakini baada ya mechi nikaenda katika vyumba vya kubadilishia nguo vya marefa ili nimuombe msamaha na nimuulize refa lakini hakutaka kuongea na mimi”

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement