Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Simba wameianza vyema safari ya kwenda Liverpool leo

on

Siku moja baada ya watani zao wa jadi Yanga SC kutolewa katika michuano ya SportPesa Super Cup 2018 dhidi ya Kakamega kwa magoli 3-1, leo ilikuwa ni zamu ya wenzao Simba SC.

Simba wakiwa Nakuru walicheza game yao ya kwanza ya mtoano dhidi ya Kariobangi Sharks lakini hakuna timu iliyofanikiwa kuruhusu goli hadi dakika 90 zinamalizika.

Baada ya hapo muamuzi akaamuru upigwaji wa mikwaju ya penati na Simba SC kuibuka na ushindi wa penati 3-2, hivyo ushindi huo unawapeleka rasmi hatua ya nusu fainali.

Ushindi huo unawafanya Simba kuanza kulinyemelea taji la Ubingwa wa michuano hiyo, ambapo wakifanikiwa kuwa Mabingwa watavuna pesa na kupata nafasi ya kwenda jiji Liverpool England katika uwanja wa Goodson Park kucheza game ya kirafiki na Everton.

Soma na hizi

Tupia Comments