Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Mpango wa Australia kuwa muuzaji nambari moja wa Bangi Duniani

on

Katika mataifa mbalimbali Duniani kumekuwa na vita ya kupinga biashara na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo Bangi kutokana na sababu mbalimbali. Sasa Serikali ya Australia imetangaza kwamba ina mpango wa kuwa muuzaji mkubwa zaidi wa bangi Duniani ambayo itakuwa inatumiwa kwa ajili ya matibabu na si burudani.

Taifa hilo linapanga kufanyia mabadiliko sheria zake na kujiunga na Canada na Uholnazi ambazo kwa sasa ndizo nchi pekee ambazo huuza bangi nje ya mipaka yao.

Waziri wa Afya Greg Hunt amesema hatua hiyo itawasaidia pia wagonjwa nchini Australia ambapo matumizi ya Bangi yaliidhinishwa mwaka 2016 kwa matibabu

“Lengo letu liko wazi: kuwapa wakulima na wenye viwanda wa Australia nafasi bora zaidi katika kuwa wauzaji nambari moja wa bangi ya kutumiwa kwa sababu za kimatibabu duniani,” -Bw Hunt

California ni jimbo kubwa zaidi la Marekani lililohalalisha matumizi ya bangi kwa ajili ya burudani huku Uruguay na Israel pia zina mipango sawa na Australia kwa ajili ya matibabu

“USIWE MSTAAFU UKAENDA KUJENGA KIWANDA UTAKUFA”- WAZIRI MWIJAGE

FULLVIDEO: BABU SEYA NA PAPII KOCHA RASMI WAINGIA STUDIO, WAZUNGUMZA HAYA

Soma na hizi

Tupia Comments