Tangaza Hapa Ad

Michezo

TOP 5: Imetajwa ya tuzo za CAF Afrika 2016 ambazo Samatta alitajwa

on

November 22 2016 shirikisho la soka barani Afrika CAF limetaja list ya majina matano yaliochaguliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2016, majina hayo matano yamechaguliwa kwa kupigiwa kura.

List hii imechaguliwa kwa kura za kamati ya vyombo vya habari inayotambuliwa na CAF na kamati ya maendeleo ya ufundi ya CAF pamoja na kamati nyingine inayohusisha watu 10. Tuzo hizo zitafanyika January 5 2017 Abuja Nigeria.

Mtanzania Mbwana Samatta ambaye mwaka 2015 alikuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi ya ndani, hakufanikiwa kuingia Top 5 katika list hiyo iliyotangazwa leo November 22 2016.

screen-shot-2016-11-22-at-8-55-53-pm

TOP ya Wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika

1. Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borrusia Dortmund)

2. Riyad Mahrez (Algeria & Leicester City)

3. Sadio Mane (Senegal & Liverpool)

4. Mohamed Salah (Egypt & Roma) 

5. Islam Slimani (Algeria & Leicester City)

screen-shot-2016-11-22-at-8-56-14-pm

Wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wanaocheza Ligi za ndani ya Afrika

1. Khama Billiat (Mamelodi Sundowns & Zimbabwe)

2. Keegan Dolly (Mamelodi Sundowns & South Africa)

3. Rainford Kalaba (TP Mazembe & Zambia)

4. Hlompho Kekana (Mamelodi Sundowns & South Africa)

5. Denis Onyango (Mamelodi Sundowns & Uganda)

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement