Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Dr Tulia alivyotoa Mil 10 kuboresha huduma za afya K’njaro

on

December 31, 2017 Naibu Spika Dr Tulia Ackson kupitia Taasisi yake ya TULIA TRUST amechangia shilingi Milioni 10, Mifuko 30 ya Cement pamoja na Lori moja la mchanga katika harambee ya ujenzi wa chumba cha Ultra Sound kwenye kituo cha Afya Kifula, Kata ya Kifula, Wilayani Mwanga, Mkoani Kilimanjaro.

Katika Katika harambee hiyo jumla ya Shilingi Milioni 32 zilipatikana kufuatia michango mingine iliyotolewa na Mfuko wa Maendeleo wa Ugweno pamoja na Wananchi, Fedha ambazo zitaweza kukamilisha ujenzi wa jengo hilo pamoja na kununua Mashine ya Ultra Sound.

Aidha, Mfuko wa Maendeleo ya Jamii wa Ugweno umeahidi pia kununua Gari la Wagonjwa kwa ajili ya Kituo hicho cha Afya.

Sababu za RC Geita kuzuia likizo za wafanyakazi

Soma na hizi

Tupia Comments