PremierBet Tanzania Usain Bonus Ad

Michezo

Sturridge aiokoa Liverpool mbele ya Chelsea

on

Baada ya mashabiki wa Man United kuondoka vichwa chini mchana wakati wa game ya Man United dhidi ya West Ham United kumalizika kwa Man United kupoteza kwa magoli 3-1, usiku ilikuwa zamu ya Chelsea na Liverpool katika uwanja wa Stamford Bridge.

Chelsea wakiwa nyumbani walianza kupata goli la mapema dakika ya 26 kupitia kwa staa wao Eden Hazard na goli hilo kudumu kwa muda mrefu, kiasi cha wengi kuamini point tatu zinabaki Stamford Bridge, wakati wengi wakiamini hivyo dakika moja kabla ya game kuisha Daniel Sturridge akafunga goli la kuisawazishia Liverpool na kuufanya mchezo kumalizika 1-1.

Sare hiyo imeifanya Chelsea kufikisha jumla ya point 17 ikiwa nafasi ya tatu nyuma ya Liverpool waliopo nafasi ya pili kwa kuwa na jumla ya point 19, wote Liverpool na Chelsea wamecheza game saba, Livepool wameshinda game 6 huku Chelsea wameshinda game 5.

Matokeo ya game za EPL September 29 2018.

Msimamo wa EPL ulivyo kwa sasa.

JB na Ray “Hata Yanga wao wanajua Simba ana timu bora”

Soma na hizi

Tupia Comments