Tangaza Hapa Ad

fB insta twitter

UTAFITI: Haya hapa Madhara ya kukaa sehemu moja kwa muda mrefu..

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipata huko.

Moja ya habari iliyoandikwa kwenye magazeti ya October 5, 2016 ni hii kutoka gazeti la Mtanzania yenye kichwa cha habari ‘Kukaa muda mrefu husababisha Saratani’

Imeelezwa kuwa watu wanaokaa kitako maofisini au kwenye foleni za magari kwa zaidi ya masaa manne wako katika hatari ya kupata magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza ikiwemo magonjwa ya Moyo, Shinikizo la Damu, Saratani na Kisukari.

Kwa mujibu wa Dr. Fredrick Mashili kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) amesema sababu kubwa inayopelekea watu kupata magonjwa hayo ni kukaa muda mrefu maofisini au kwenye foleni na kutofanya mazoezi baada ya kutoka makazini.

Akitolea mfano wa ripoti ya hivi karibuni kutoka Shirika la Moyo la Marekani lilichapisha makala yenye kichwa cha habari “International Cardiovascular Desease Statistics” limeeleza kuwa kutofanya mazoezi na kula vyakula visivyofaa ni moja ya mambo yanayochangia kwa kiasi kikubwa magonjwa hayo.

Dr. Mashili ameeongeza kuwa kukua kwa Teknolojia kumechangia watoto kukosa muda wa kucheza badala yake hupendelea kukaa na kucheza michezo ya kwenye kompyuta na video (Gaming), tatizo ambalo ni kubwa kwao kwasababu hupelekea watoto kutojiheshimu, kuwa na wasiwasi mwingi na kufadhaika kila wakati.

ULIPITWA NA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV? TAZAMA HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement