PremierBet Tanzania Usain Bonus Ad

Michezo

Staa wa Man City kafungiwa kuendesha gari England

on

Moja kati ya stori zinazochukua headlines katika soka ni pamoja na hii ya beki wa kati wa club ya Man City ya England Benjamin Mendy kutangazwa kufungiwa miezi 12 kuendesha gari na kupunguziwa point 24 katika leseni yake.

Benjamin Mendy amekubali makosa manne ikiwemo la kushindwa kuthibitisha dereva aliyekuwa anaendesha Merceds Benz yake, ambapo imekuwa ikituhumiwa kuendeshwa kwa speed katika matukio manne tofauti.

Adhabu ya Mendy inaenda pamoja na faini ya Pound 2500 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 5, Mendy hakuweza kuhudhuria Mahakamani leo zaidi ya kuwakilishwa na mwanasheria wake Gwyn Lewis kwa niaba yake, Benz ya Mendy ilionekana kufanya makosa hayo February 8, 9 na mara ya tatu na nne ikiwa ni February 21.

EXCLUSIVE: Licha ya kuwa na pesa na ustaa, hii ndio Sababu inayomfanya Samatta asiringe

Soma na hizi

Tupia Comments