Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: Shirikisho la vyuo vikuu lataja hujuma bodi ya mikopo

on

Wakati suala la mikopo ya elimu ya juu likizidi kuchukua headline, Leo November 02 2016 Shirikisho la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu Tanzania limetoa siku saba kwa serikali kushughulia changamoto mbalimbali zinazowakabili wanafunzi kuhusu mikopo.

Aidha Shirikisho hilo kupitia katibu msaidizi wa shirikisho hilo, Daniel Zenda amezungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam na kuzitaja baadhi ya hujuma ambazo anadai zinafanywa kwa makusudi na watendaji kutoka bodi ya mikopo ili kumkwamisha Rais John Magufuli.

>>>’Tunasikitishwa sana juu ya hujuma zinazoendelea kule bodi ya mikopo na tumehuzunishwa kwa kiwango kikubwa baada ya sakata hili la mikopo kuchukua taswira mpya ndani ya nchi, ambayo haipendezeshi sekta ya elimu, kwa hiyo tumejiridhisha kuwa kuna hujuma zinafanyika dhidi ya serikali ili kumkwamisha Rais Magufuli’;-Daniel Zenda

>>>’Miongozo kutoka bodi ya ya mikopo na mwingine kutoka Wizara ya Elimu, hii miongozo inakinzana, athari ya kupingana kwa hii miongozo inapelekea wanafunzi wengi kukosa mikopo, kigezo cha umri hakipo katika miongozo yote miwili lakini kule bodi ya mikopo kinatumika sisi tunaona ni hujuma mojawapo’;-Daniel Zenda

>>>’Miongozo yote miwili inasema yatima watapata mikopo lakini kuna yatima UDSM wasiopungua 64 na wana division I na  II lakini hawajapata mikopo, Chuo cha Mwalimu Nyerere kuna wanafunzi zaidi ya 78′;-Daniel Zenda

ULIKOSA HII YA WASAMARIA  WAVYOMFUTA MACHOZI MWANACHUO WA UDSM ALIYEONEKANA AKILIA GAZETINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement