Airtel TZ - Winky Music
Ads Separator
Clouds - Tunakufungulia Dunia
Home » General News » Ule ugeni kutoka Himaya ya Kifalme Uingereza umekutana na mastaa wengine Marekani, picha zipo hapa…

January Makamba - Tanzania Mpya

Ule ugeni kutoka Himaya ya Kifalme Uingereza umekutana na mastaa wengine Marekani, picha zipo hapa…

Close-Up of HandshakeVyombo vikubwa vya habari Duniani pamoja na mitandao ya kijamii viliripoti kuhusu ziara ya siku tatu inayofanywa na mjukuu wa Malkia Elizabeth, Prince William na mke wake Kate Middleton huko Marekani na tukapewa taarifa siku ya jana pia kwamba ugeni huo ulipata nafasi kuingia ndani ya Ikulu ya Marekani kwa mara ya kwanza na Prince akafanya mazungumzo na Rais Obama.

Habari kubwa kwa sasa ni kuhusiana na wawili hao siku ya jana kuhudhuria mechi ya Basketball na kuushuhudia ushindi wa Cleveland Cavaliers dhidi ya Brooklyn Nets na kupata nafasi ya kukutana na staa wa Basketball LeBron James, Jay Z pamoja na Beyonce.

Walipata nafasi ya kupiga stori kidogo na mastaa hao baada ya mechi hiyo kuisha.

PW

Prince William, Kate, Jay Z na Beyonce wakisalimiana baada ya kukutana katika Ukumbi wa Barclays Centre ilipokuwa ikichezwa mechi ya Basketball kati ya Cleveland Cavaliers na Brooklyn Nets jana Desemba 09.

PW I

PW II

Waandishi wa Habari wakipiga picha wakati Prince na mkewe walipokutana na Jay Z na Beyonce.

PW III

Prince William, Kate na LeBron James.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tags :
Previous post link
Next post link
Scroll To Top