Michezo

“Sasa hivi natukanwa naambiwa mimi Simba SC”-Edo Kumwembe

on

Mchambuzi wa masuala ya soka Edo Kumwembe amekuwa miongoni mwa watanzania wengi wanaopenda kuandika mawazo yao kupitia mitandao ya kijamii, Edo Kumwembe hajawahi kuweka wazi rasmi yeye ni timu gani kwa hapa Tanzania au nje ya Tanzania lakini watu wamekuwa wakimtuhumu kwa nyakati tofauti kuwa yeye yupo timu fulani

Kupitia ukurasa wake wa instagram amepost ujumbe unaonesha kuwa watu wamekuwa na tabia za kupenda kumkosoa akimsifia mchezaji wa Yanga na kumuita yeye Yanga na akisifia mchezaji wa Simba SC anakosolewa na kuambiwa yeye Simba, leo ameandika hivi kupitia ukursa wake wa instagram kitu ambacho kinamchanganya kuwafahamu watu wanataka nini.

 

“Labda sijui soka labda sina unafiki sometimes kuna mambo yanamoponza mtu msemakweli, zamani nilikuwa naambiwa mimi Yanga kwa sababu ya post kama hizo za kuwasifia wakiwa Tshishimbi na pia wakina Kamusoko kabla ya hapo rafiki yangu @hajismanara alikuwa ananiambia mimi Yanga “>>>Edo Kumwembe

“Siku hizi nakoshwa na akina Kagere akina Chama nawapost mara nyingi zaidi haniambii kama mimi Simba amekaa kimya nimejifunza kuwa hivi, nimejifunza katika kuamini ninachofikiri napenda mpira kuliko timu au itikadi zama huwa hazidanganyi, sasa hivi natukanwa naambiwa mimi Simba Sijali”>>>Edo Kumwembe

MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe

Soma na hizi

Tupia Comments