Michezo

Simba SC sasa wamemalizana na Mbabane 8-1

on

Mabingwa Tanzania Club ya Simba SC leo December 4 2018 walikuwa uwanjani mjini Mbabane Swaziland kucheza dhidi ya Mbabane Swallows mchezo wa marudiano wa CAF Champions League baada ya mchezo wa kwanza kucheza Dar es Salaaam wiki iliyopita uwanja wa Taifa.

Simba ambao mchezo wa kwanza uwanja wa Taifa walishinda magoli 4-1, leo wamefanikiwa tena kurudia ushindi wa magoli manne safarii hii mchezo ulimalizika kwa magoli 4-0, hivyo Simba wanatinga round inayofuata kwa kuifunga Mbabane kwa aggregate ya jumla ya magoli 8-1.

Magoli ya ushindi ya leo ya SImba SC yamefungwa na Chota Chama dakika ya 28 na 33, Emmanuel Okwi dakika ya 52 na mwisho Meddie Kagere dakika ya 63, SImba sasa wamepita round ya kwanza wanasubiri kujua watacheza na timu gani round inayofuata wakati huu wakipambania kuingia hatua ya Makundi.

MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe

Soma na hizi

Tupia Comments