PremierBet Tanzania Usain Bonus Ad

Michezo

Ronaldo anaweza kupoteza Tsh Tirioni 2

on

Ni siku kadhaa sasa zimepita tokea nahodha wa timu ya taifa ya Ureno anayeichezea club ya Juventus ya Italia Cristiano Ronaldo akumbane na kashfa ya tuhumza za ubakaji wa mwanamke Kathryn Mayorga nchini Marekani.

Iliripotiwa kuwa Ronaldo anatuhumiwa kutenda kosa la kumbaka mwanamke huyo mwaka 2009 akiwa Las Vegas Marekani na alilazimika kumpa hela ili abaki kimya asitoe taarifa hizo kwa umma.

Kathryn Mayorga

Sasa baada ya kashfa hiyo kusambaa kampuni ya Nike ambayo ina mkataba na Ronaldo, inaeleza kuwa kama Ronaldo atakutwa na hatia katika tuhuma hizo basi itasitisha nae mkataba wao wa kibiashara dhidi yake.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 33 na mshindi mara tano wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d’Or amekuwa na mkataba na Nike toka mwaka 2003 na mwaka 2016 alisaini mkataba ambao akataja kuwa maisha wenye thamani ya dola bilioni 1, hivyo kama dili hilo litavunjika Ronaldo atapoteza zaidi ya Tsh Tirioni 2.

“Simba tumewaachia, sisi hatuna presha”-Kocha wa Yanga

Soma na hizi

Tupia Comments